Chanjo hiyo itatolewa kwa wasichana waliofikisha umri wa miaka 14 Unguja na Pemba.
Kwa mujibu wa Ofisa wa Kitengo cha chanjo Wizara hiyo, Abdulhamid
Ameir Saleh,lengo la kutolewa kwa chanjo hiyo ni kupunguza saratani ya
mlango wa kizazi kwa asilimia 80 katika kipindi cha miaka mitano.
Alisema,ili kupata kinga kamili,walengwa watahitaji kupata dozi
mbili ambapo ya pili itatolewa miezi sita baada ya kupata ya dozi ya
kwanza.
Alisema, chanjo hiyo ya HPV inakinga maambukizi ya virusi vinavyosababisha saratani ya mlango wa kizazi.
“Chanjo hii inaweza kupunguza matukio ya saratani ya mlango wa kizazi kwa kiwango kibwa,” alisema.
Alisema, chanjo hiyo ni salama,imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Alisema, walengwa wote watasajiliwa na kupata kadi maalum
inayothibitisha kuwa amepata chanjo na kadi hiyo itaonyesha tarehe ya
kurudi kwa dozi ya pili na ambayo mlengwa amekamilisha ratiba yake ya
chanjo.
Chanjo ya HPV inawakinga mabinti dhidi ya saratani ya mlango wa
kizazi hapo baadaye na ni salama ,haina madhara na haimzuii binti
kutopata watoto.

chanzo: zanzibarleo.
Comments