Siku ya leo ya tarehe 13 Farvardin (Aprili Pili) ni miongoni mwa siku bora za Sikukuu ya mwaka mpya ya Nouruzi ambayo katika kalenda rasmi ya Iran inajulikana kama Siku ya Maumbile na ni moja ya siku rasmi za mapumziko hapa nchini.
Baada ya kupita siku 12 za mwaka mpya wa 1397 hijria shamsia, Wairani, wakiandamana na jamaa wote wa familia hupitisha siku ya 13 ya mwaka kwenye maeneo ya wazi ya mandhari za maumbile kwa ajili ya kujichangamsha na kujiburudisha.
Watu wa Iran wanaichukulia desturi hiyo ya kuadhimisha siku ya 13 ya Sikukuu ya Nouruzi kuwa ni kuonyesha ushukurivu kwa neema za Mwenyezi Mungu na kwamba kuyaangalia maumbile ya msimu wa machipuo yaliyohuika tena upya baada ya msimu wa baridi kali ni sawa na kushuhudia alama ya Kiyama na kufufuliwa viumbe.
Kwa sababu hiyo katika siku hii ya mwisho ya mapumziko ya Nouruzi huwa wanaamua kutoka majumbani na kuelekea kwenye maeneo ya maumbile.
Baadhi ya watu wanaamini kuwa, kujumuika pamoja jamaa wote wa familia katika maeneo ya mandhari za maumbile ndio upeo wa juu kabisa wa raha na burudani katika siku za mapumziko ya mwaka mpya.
chanzo:parstoday.
Comments