Iran yabadilisha rasmi matumizi ya Euro badala ya Dola katika miamala yake ya kigeni.

Iran yabadilisha rasmi matumizi ya Euro badala ya Dola katika miamala yake ya kigeniBaraza la Mawaziri la Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lililokutana jana (Jumatano) likiongozwa na Rais Hassan Rouhani lilitangaza rasmi kubadilisha miamala yake ya kigeni kutoka Dola kwenda katika Euro.

Ofisi ya Rais Rouhani imetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, kuanzia sasa wizara zote, taasisi na mashirika yote ya serikali ya Iran yatakuwa yanatumia Euro kama msingi wa fedha za kigeni za ripoti, takwimu, taarifa na data zake za fedha za kigeni.
Kwa mujibu wa maamuzi hayo ya serikali, Benki Kuu ya Iran imewajibishwa kuanzia tarehe ilipotoka amri hiyo, kuangalia thamani ya Rial ya Iran kwa kuilinganisha na Euro na iwe inasimamia na kutoa taarifa za mara kwa mara kuhusu suala hilo.
Katika siku za hivi karibuni fedha za kigeni nchini Iran zilikuwa zinapanda kiholela, suala ambalo limeifanya Serikali kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na wimbi hilo kama vile kutangaza bei moja ya fedha ya kigeni na kupiga marufuku bei nyingine zote.
Katika hotuba yake ya jana mbele ya waziri, maafisa na wafanyakazi wa Wizara ya Usalama wa Taifa ya Iran, Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema: 
Tunapoyaangalia kwa umakini na kwa kina zaidi masuala haya (ya kupanda kiholela thamani ya fedha za kigeni humu nchini) tutaona wazi namna taasisi na mashirika ya kijasusi ya maadui yalivyohusika.
chanzo:parstoday

Comments