Akizungumza na uongozi wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake
na Watoto, Mkurugenzi wa Shirika hilo kanda ya Afrika Mashariki,
Walington Chibebe ambae amefika ofisini Mwanakwerekwe kujitambulisha,
alisema ataendeleza programu hizo ambazo ni pamoja na kuendeleza mafunzo
ya kazi za uanagenzi kwa watafuta kazi vijana.
Alisema tayari ameziangalia na kuzipitia programu tafauti ambazo
amezikuta katika ofisi yake ambazo zimeachwa na mtangulizi wake kwa azma
ya kuimarisha maendeleo ya jamii.
“Tushirikiane ndio jambo muhimu katika kutekeleza majukumu tuliojipangia kwa faida ya jamii, wazee na vizazi vijavyo,” alisema.
Nae Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto, Maudline
Castico, alilishukuru shirika hilo kwa mchango wake katika kusaidia
masuala mbali mbali ikiwemo uanzishwaji wa pensheni jamii kwa wazee,
sambamba na kituo cha kulea na kuendeleza ujasiriamali kilichopo Mbweni
ili kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana nchini.
Alisema ukosefu wa ajira hasa kwa vijana nchini bado ni tatizo
linalohitaji kupatiwa ufumbuzi wa kudumu hivyo aliliomba shirika hilo
kusaidia katika eneo hilo ili kuwajengea uwezo vijana na wananchi ili
waweze kujiajiri wenyewe na kuendeleza maisha yao.
chanzo: anzibarleo.
Comments