HRW: Mamluki wa Imarati wanawabaka wahajiri wa Kiafrika Yemen.

HRW: Mamluki wa Imarati wanawabaka wahajiri wa Kiafrika YemenShirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema mamluki wanaofadhiliwa na kuungwa mkono na Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Yemen wanawabaka na kuwalawiti wahajiri wa kike na kiume raia wa Afrika katika nchi hiyo masikini ya Kiarabu.

Bill Frelick, Mkurugenzi wa Haki za Wakimbizi wa Human Rights Watch amesema, maafisa usalama wenye mahusiano na Imarati nchini Yemen wamekuwa wakiwabaka na kuwalawiti kwa makusudi na kwa mpangilio maalumu wahajiri wanaume na wanawake, wakiwemo watoto wadogo wa Kiafrika, kabla ya kuwarejesha kwa nguvu katika nchi zao.
Shirika la Uhamiaji Duniani IOM limesema wahajiri wapatao 87, 000 wa Afrika waliingia nchini Yemen kupitia usafiri wa boti kutoka nchi za Pembe ya Afrika mwaka jana 2017 pekee.
Haya yanajiri katika hali ambayo, gazeti la al-Quds al-Arabi hivi karibuni liliripoti kuwa, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu zinataka kuwasajili maelfu ya vijana wa Kiafrika hususan kutoka nchi za Chad na Uganda, zitakaowatumia kama mamluki katika operesheni zao za nje ya nchi vikiwemo vita dhidi ya Yemen. 
Tayari mamia ya mamluki raia wa Sudan waliokodishwa na Saudia na Imarati wameuawa kufikia sasa katika uvamizi wa muungano wa kijeshi unaoongozwa na Riyadh dhidi ya jirani yake Yemen.
chanzo:parstoday.

Comments