
Akizungumza wakati wa kutembelea Eneo hilo
kwa kuangalia athari za Mazingira zilizojitokeza ikiwa ni muendelezo wa
ziara zake Unguja, Mh.Samia amesema hali ya Mazingira katika bonde hilo
hairidhishi jambo ambalo linaweza kuleta athari mbalimbali kwa wananchi
ikiwemo kupanda kwa maji ya chumvi katika makaazi ya watu.
Amesema kuna maeneo yameshapata athari
za Uharibifu wa mazingira na kusababisha kukatika kwa shughuli za
kijamii ikiwemo kilimo lakini kutakapo andaliwa mazingira maalumu ya
kuchimba mchanga itawapa fursa wananchi kuendelea na shughuli zao za
kuimarisha Uchumi.
Aidha ametowa wito kwa wasimamizi wa Eneo
hilo kuchimba Mchanga kwa kuzingatia athari za mazingira pamoja na
kufukia Mashimo ya Mchanga ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza
hususani kwa watoto wanaotembelea Eneo hilo.
Kwa Upande wake Waziri wa kilimo maliasili
mifugo na Uvuvi Rashid Ali Juma amesema tayari Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar inaendelea na jitihada ya kulinda mazingira katika eneo hilo
baaada ya kuchimbwa mchanga ikiwemo kupanda miti ili kuirejesha ardhi
katika hali Nzuri.
Amesema katika kukabiliana na tatizo hilo
pia wameandaa utaratibu maalumu wakuchimba mchanga katika eneo hilo
pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria wachimbaji wanaochimba kinyume
na sheria ili kudhibiti uharibifu wa mazingira.

Amesema Vijana ni Nguvu kazi ya taifa
wanaochangia maendeleo ya Nchi hivyo watakapo shirikishwa wataepukana na
vikundi hatarishi vitavyoharibu amani ya Nchi.
Amesema kutokana na vijana kuwa na Mwamko
wa Kujituma katika Shughuli za Chama na Serikali hivyo watakapo pewa
kipaombele wataweza kuwa walinzi wa Chama cha Mapinduzi pamoja na
kukisaidia Chama kupata Ushindi katika Uchaguzi wa Mwaka 2020.
Mjumbe huyo amekagua mradi wa maduka ya
Biashara CCM Nungwi Mkoa wa Kaskazini na kuona mipango ya kujiimarisha
kiuchumi,Amefungua ofisi ya Chama cha CCM Donge ,ametembelea eneo
lililoathirika mazingira Donge Chechele na kufungua Jengo la Ofisi ya
CCM Mkoa wa Kaskazini Mahonda pamoja na kupokea taarifa za chama hicho.
Comments