Dc Micheweni : Madawa yakulevya yanaepukika.

Image result for dc micheweniNa Othman Ali Juma.
Mkuu wa Wilaya Micheweni Mh. Salama Mbarouk Khatib amesema mapambano dhidi ya madawa ya  kulevya na ulawiti ndio kipao mbele kwa mwaka huu ili kuweza kuwanusuru vijana,  ambao ndio waathirika wakubwa wa matendo hayo.

Ameyasema hayo huko katika skuli ya Elimu mbadala Wingwi  Wilaya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati akifungua mafunzo maalum kwa vijana wa wilayani humo yaliyo andaliwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Mikunguni ( MYDO) yenye lengo la kutoa hamasa kwa vijana kujiunga na vyuo vya amali ili kuondokana na halingumu za kimaisha pamoja na utegemezi wa ajira serekalini.

Amesema wilaya yake imekuwa na idadi kubwa ya matendo maovu ikiwa nipamoja na ulawiti na utumiaji wa madawa yakulevya ikilinganishwa na wilaya nyengine Pemba hali ambayo imepelekea kundi kubwa la vijana ambao ndio tegemeo la Taifa kuathirika kiafya nahata kisaikolojia.

Amesema kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nahata Polisi janmii watahakikisha wanadhibiti matumizi, uuzaji na uingizaji wa madawa ya kulevya katika wilaya hiyo.

"Vijana wote wanajihusisha na utumiaji, uuzaji na uingizaji wa madawa tunakula nao sahani moja"Alisema Dc Salama.

Amefahamisha kuwa nijuzi maeneo ya msasani wameweza kufanikiwa kukamata jumla ya madumu (28) ambayo ni maroeko kwa ajili ya upikaji wa pompbe za kienyeji sambamba na mitaimbo ya kupikia pombe hizo.

"Juzi majira ya saa 4 usiku tulikamata madumu 12 na asubuhi yake tulifanikiwa kukamata tena madumu 16".Alisema.

Aidha amewataka wananchi wa wilaya hiyo kutoa mashirikiano yao yadhati kwa kutoa taarifa pindi wanapoona vitendo hivyo vikiendelea huku akisema kuwa micheweni bila madawa ya kulevya inawezekana.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Mabaraza ya vijana Wilaya ya micheweni Pemba Nd. Ali Suleiman Shaame amewataka vijana kuacha kukaa maskani na kufanya matendo yaliyokuwa hayaleti maendeleo na badala yake kujiunga na mabaraza hayo ili kuweza kuunga nguvu ya pamoja kwa kubuni miradi itakayo wasaidia katika maisha yao.

"Kijana akiendelea kukaa maskani maranyingi hushawishika na kujiingiza katika vitendi viovu, matuzi ya madawa ya kulevya, ulawiti na matendo mengine maovu, musingoje kufikia huko njooni mujiunge na mbaraza haya tunufaike na fursa zilizomo".Alisema.

Hatahivyo amewataka  vijana kutokaa tu ovyo watafute kazi zakufanya zitakazo wasaidia kupata rizki zao za halali.

Comments