
Waziri wa Afya
Zanzibar Hamad Rashid Mohamed ameyasema hayo alipozindua Bodi ya
Wakurugenzi ya Taasisi hiyo huko katika Ukumbi wa Wizara ya Afya, Mnazi
mmoja mjini Zanzibar
Amesema tafiti za Afya ni jambo muhimu kwa taifa na taasisi hiyo itakuwa na jukumu la kulinda afya za Wananchi hao.
Amefahamisha kuwa
Taasisi hiyo itakuwa na majukumu tofauti ikiwemo kuisadia jamii
kubadili mtazamo wake katika mambo mbalimbali ambapo Taasisi inaweza
kuanzia kwa kujikita zaidi kwa Wanafunzi wa ngazi tofauti.
“Tutakapofanya
tafiti tuhakikishe kuwa kipaumbele kinakuwa kwa wanafunzi wa Skuli na
Vyuo ambao watakuwa mabalozi wazuri wa leo na kesho” alisema Waziri
Hamad.
Amesema serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini sana afya za wananchi wake na kutoa
pongezi kwa Rais wa Zanzibar Dkt. Shein kwa muono wake thabiti wa
kuanzisha Taasisi hiyo.
Waziri Hamad
amefahamisha kuwa Wizara yake inatambua umuhimu wa kuwepo kwa vifaa vya
kisasa na vya kipekee katika maabara ya taasisi hiyo na kuahidi
kufanikisha ipasavyo.
Aidha ameahidi kuwapatia vijana elimu endelevu na kuwajengea uwezo katika nyanja za kitafiti Zanzibar.
Ametoa wito kwa Bodi hiyo kujifunza kutoka Taasisi zingine za Kitafiti Tanzania na nje ya Tanzania ili kukuza uwezo wake.
Kwa upande wake
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Asha Abdulla amefahamisha kuwa maabara ya
Taasisi hiyo itakuwa na kazi nyingi za kufanya katika uchunguzi wa
magonjwa ya kibinadamu na pia itashiriki katika tafiti za uvumbuzi wa
dawa mpya zinazotokana na mimea kwa kutumia utaalamu wa kisasa.
Amefahamisha kuwa
tunaamini kuwa kuna mimea mingi ya dawa za asili Zanzibar ambazo
zimetumika toka enzi na sasa wakati umefika wa kuzifuatilia kwa ukaribu
ili kupata ufanisi na usalama wa dawa hizo.
Kwa upande wa
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Saleh Mohd Jidawi amesema Taasisi ya Maswala ya
Utafiti wa Afya Zanzibar ilianza rasmi Januari 2, 2018 ambapo kuundwa
kwake kunatokana na “Legal Notice” No. 125 chini ya kifungu 53 cha
Katiba ya Zanzibar.
Akitaja
majuku ya Taasisi hiyo Jidawi amesema ni pamoja na kuratibu na kukuza
utafiti unaolenga kutafuta suluhu kwa matatizo ya magonjwa katika jamii
ya Zanzibar.
Jukumu jingine ni
kusimamia na kusajili tafiti zote za afya zinazofanyika Zanzibar na nje
ya Zanzibar kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Taasisi itahusika
pia na mahusiano na taasisi za kimataifa katika masuala yanayohusu
tafiti za afya na kuwasaidia Wanasayansi wa kizanzibari kuingia katika
mahusiano ya kimataifa ya tafiti za afya kwa faida za Wazanzibari.
Hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo wa Wizara ya afya.
ZANZIBAR24
Comments