Abdul
Nondo, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye
anakabiliwa na kesi ya kujiteka mwenyewe, mzazi wake Omar amethibitisha
kuwa baba yake alizaliwa mwaka 1919 huko Ujiji, Kigoma na kuwa ni
miongoni mwa waasisi wa chama cha Tanu.
Mzee Omar, alisema baba yake huyo aliyemtaja kwa jina la Omar Kagobe alipata watoto 30, mmoja akiwa yeye.
“Nashangaa
hao wanaomkamata na kumhoji mtoto wangu kuwa sio raia, wananichekesha
sana kwa kuwa najua mwisho wa siku watajua ukweli wake. Ukweli ni kwamba
wazazi wangu ndio waasisi wa Tanu na walishiriki kikamilifu katika
kupigania uhuru wa nchi hii, hivyo suala hilo halinipi wasiwasi wala
hofu na hivyo vyeti wanavyovitaka mbona vipo tu, ila waelewe kuwa sisi
ni Wamanyema halisi na ni raia halali wa nchi hii,” alisema.
Naye
Mwenyekiti wa ACT - Wazalendo, Mkoa wa Kigoma, Sendwe Mbaruku, alitoa
taarifa Alhamisi kuhusu suala la Nondo kuhojiwa na uhamiaji na kusema;
“Kijana Abdul ni mtoto wetu hapa Kigoma, wazazi wake ni wakazi na wapiga
kura wa hapa Ujiji, zaidi ni Watanzania wenzetu.”
Maelezo
haya yametolewa na mzazi huyo Siku chache baada ya Mwenyekiti wa
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo kuhojiwa na Idara ya
Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam kuhusu uraia wake.
Mzazi
huyo amesema babu yake Nondo, alishawahi kuwa Polisi kwa miaka 18
kuanzia mwaka 1940 hadi 1958 na alishafanya kazi huko Mabatini mkoani
Mwanza na sehemu nyingine za nchi.
Alisema
babu yake wakati akiwa polisi, ndipo zilipoanzishwa Kota za Msimbazi,
Dar es Salaam na jina lake lilikuwa maarufu, akijulikana kama Mzee
Kagobe.
Kama
haitoshi alisema bibi yake Nondo alikwenda kuhiji, mnamo 1970 na
alipewa hati ya kusafiria ya Tanzania, huku akihoji, “Kama angekuwa sio
raia wa Tanzania angepewaje hati hiyo?”
Baada
ya Nondo kuripoti polisi mjini Mafinga alishikiliwa na jeshi hilo Mkoa
wa Iringa na baadaye kukabidhiwa kwa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam.
Kamanda
wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa alisema kupitia uchunguzi wa kisayansi,
wamebaini kuwa hakuwa ametekwa, bali alijiteka na tayari suala lake
lipo mahakamani, Iringa.
chanzo:Mpekuzi.
Comments