Afariki akiogolea baharini.

MTU mmoja amefariki dunia katika pwani ya Bambuu iliyopo Bububu baada ya kuzama wakati akiwa akiogelea pamoja na wenzake.

Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake Madema,  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali, aliesema marehemu ametambuliwa kwa jina la Omar Pauli Ziota (25) mkaazi wa Kibweni.

Alisema tukio hilo limetokea Aprili 4 mwaka huu saa 12:30 jioni ambapo kijana huyo alikuwa na wenzake wakiogelea.

Aidha alisema mwili wa marehemu umefikishwa hospitali ya Mnazimmoja kwa ajili ya uchunguzi wa kidaktari na kukabidhiwa jamaa zake kwa mazishi.

Wakati huo huo alisema Aprili 6 mwaka huu saa 8:40 mchana Mfenesini, nyumba ya Khamis Ussi Machano (38) imeungua moto na kuunguza chumba kimoja pamoja na vitu vyote vilivyomo chumbani humo.

Alisema vitu vilivyoungua vinakisiwa kuwa na thamani ya shilingi 1.7 milioni ambapo chanzo cha moto huo bado hakijajulikana huku upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea.

Chanzo: zanzibarleo.

Comments