
Adhabu hizo zilitolewa kwa timu ya Black sailors, Miembeni city na
kilimani city ambapo kila timu inalazimika kulipa faini ya shilingi laki
moja mara baada ya kubainika kutenda kosa hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari za michezo visiwani Zanzibar
Afisa habari wa chama cha soka visiwani Zanzibar ZFA Ali Bakari cheupe
alisema ZFA imezitoza faini ya shilingi laki moja kwa kila timu
kutokana na kubainika kufanya kosa la kuingia uwanjani kinyume na mlango
uliopangiwa kuingilia wachezaji ambapo vitendo hivyo vimekithiri
kufanywa na timu nyingi visiwani Zanzibar.
“ kwa mujibu wa kanuni za kuendeshea mashindano ni marufuku kwa
timu kupita katika milango ambayo haiusiki kuingilia uwanjani hivyo ZFA
imefiakia maamuzi hayo ili kukomesha vitendo hivyo vinavyofanywa na
baadhi ya timu ambavyo vinaonekana vimekithiri” alisema cheupe afisa
habari wa ZFA.
Vitendo vya timu mbali mbali kukaidi kuingilia uwanjani kupitia
mlango usiostahiki huwa unahusishwa na Imani za kishhirikina katika
soka.
Pia alisema kwa upande mwingine chama cha mpira wa miguu viwani
Zanzibar ZFA kimemchukulia hatua za nidhamu kocha msaidizi wa timu ya
kilimani city Abrahamani Mussa kutokana na kosa la kuwatolea maneno ya
kashfa waamuzi waliochezesha mchezo kati ya timu ya kiliamni city dhidi
ya black sailors.
Aidha alisema ZFA imefikia maamuzi ya kumtaka kocha huyo msaidizi
wa kilimani city kuto kaa kwenye benchi la ufundi kwa muda usiojulikana
mara baadaya kubainika kuwa ametenda vitenda vitendo vya utovu wa
nidhamu kwa kuwatolea maneno ya kashfa waamuzi.
Hata hivyo alisema pindi kocha huyo atakapo kaidi kutumikia adhabu
hiyo aliopatiwa chama cha soka visiwani Zanzibar (ZFA) basi timu nzima
kiliamani city itawajibika.
“kitendo kilichofanywa na Abrahamani mussa kocha wa kilimani city
ni kinyume na maadili ya kocha hivyo kwa maamuzi yaliochukuliwa na ZFA
ni kama onyo Kali ili mwingine asije fanya kosa kama hilo” alisema
cheupe.
Vitendo vya utovu wa adabu vimekuwa vikiripotiwa kwa wingi katika soka la Zanzibar ambapo hulitia dosari soka visiwani humo.
chanzo:
Zanzibar24.
Comments