
Sifa hizo zitaepelekea Wadau kutoka nje ya
Zanzibar kuja kujifunza namna Wakala huo unavyofanya kazi za kulinda na
kuimarisha afya ya jamii kwa maslahi mapana ya taifa.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed
ameyasema hayo wakati akizindua Bodi ya Ushauri wa Wakala huo katika
ofisi za ZFDA Mombasa mjini Zanzibar.
Amesema kinachohitajika katika Wakala huo ni kujiamini na kusimamia sheria ambazo zimewekwa kwa ajili ya kumlinda mtumiaji.
Amewasisitiza Watendaji wa ZFDA kuzikamata
na kuziangamiza bidhaa zote zisizokidhi viwango hadaharani na kwa mujibu
wa Idadi waliyoitangaza ili kuondoa tuhuma ambazo baadhi ya wananchi
huzitoa.
amesema yapo madai kwamba wanakamata bidhaa
lakini wanapoziteketeza wananchi hawapewi taarifa kamili ya
ueteketezwaji huo hivyo akasisitiza taarifa kutolewa kwa uzito wake.
Amewanasihi kuwa wanakabiliwa na majukumu
kubwa ya kuhakikisha Vyakula, Dawa na Vipodozi vinavyoingizwa vinakuwa
katika hali ya ubora ili kuepuka jukumu kwa maslahi yao ya hapa duniani
na kesho mbele ya Mungu.
“Mnajukumu kubwa mbele ya Mungu mkiruhusu mali na bidhaa mbovu mtaenda kuwajibika siku ya malipo”aliwanasihi Waziri wa Afya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya
Ushauri ya ZFDA Mayasa Ally Salim amesema utaratibu wa udhibiti
unafanywa kupitia idara nne za wakala zikiwemo Idara ya usalama wa
chakula, Idara ya Dawa Vipondozi na bidhaa za tiba, Idara ya Huduma za
maabara na Idara ya human a wakala.
Amesema kazi kubwa ya ZFDA ni kulinda na
kuimarisha afya ya jamii kwa kusimamia udhibiti wa bidhaa za chakula,
Dawa, Vipodozi, Vifaa Tiba na Vitendanishi kupitia usajili, ukaguzi na
uchunguzi wa kimaabara.
Awali akimkaribisha mgeni Rasmi Mkurugenzi
wa ZFDA Burhan Othman Simai alimuhakikishia kuwa Idara yake ipo tayari
kufua kila ushauri ambao utazidikuleta ufanisi kwa kazi yake.
Wakati huo huo ZFDA ilipokea Msaada wa Gari
mbili zenye thamani ya Shilingi Milioni 150 kutoka Mfuko wa Kimatifa
wa Global Foundation ambazo zitatumika kwa ajili ya kufuatilia
usajili,ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara kwa Unguja na Pemba.
chanzo:Zanzibar 24.
Comments