Wazanzibar wametakiwa kuzitumia fursa za kibiashara kutangaza biashara wanazozalisha ili kupata wawekezaji.

Wazanzibar wametakiwa kuzitumia fursa za kibiashara na uwekezaji zilizokuwepo nchini ili  kukuza uchumi na kujikwamua na umasikini unaowakabili wananchi wengi hususani mtu mmoja mmoja.

Akizungumza  na waandishi wa habari Meneja mauzo na masoko wa shirika la magazeti ya serikali Tanzania TSN Januarus Sebastian Maganga  amesema tarehe 16 Murch  TSN Imeandaa kongamano la kibiashara Zanzibar kwa ajili ya kuibua fursa za kibiashara kwa wafanyabiashara hasa  wafanyabiashara wadogo ambao ni wajasiriamali ili kuwasaidia katika kuonesha biashara zao kwani katika kongamano hilo kutakuwa na wawekezaji.

Amesema TSN imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia wafanyabiashara katika mikoa mbalimbali Tanzania ikiwa na lengo la kupambana na umaskini unaowakabili wananchi wenye kipato cha chini.

Maganga amesema  katika kuelekea katika uchumi wa Viwanda Tanzania serikali imekusudia kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kutafuta wawekezaji kuwekeza nchni  pamoja na kuwainua wafanyabiashara biashara wadogo ili kwenda sambamba na lengo la Tanzania kuondokana na umaskini.

Aidha ametoa wito kwa wajasiriamali mbalimbali kushiriki pamoja na wananchi  ili kuweza kutangaza biashara zao wanazozalisha kwa kutumia rasilimali  za asili.

Kongamano hilo linalotarajiwa kuhuzuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano Tanzania pamoja na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambalo linatarajiwa kufunguliwa na Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani.

Chanzo:Zanzibar24.

Comments