Wamarekani wengi wapinga sera za Trump kuhusu Iran.

Wamarekani wengi wapinga sera za Trump kuhusu IranUchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya Gallup umebaini kuwa, asilimia kubwa ya Wamarekani hawakubaliani na siasa za Rais wa nchi hiyo, Donald Trump dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Taasisi ya uchunguzi wa maoni ya Gallup yenye makao yake nchini Marekani imewahoji Wamarekani kuhusu Iran na siasa za serikali ya nchi hiyyo kuhusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 
Katika uchunguzi huo, taasisi hiyo iliwauliza Wamarekani iwapo wanaunga mkono siasa za serikali ya Marekani kuhusu Iran au la. 
Matokeo ya uchunguzi huo yanaonesha kuwa, asilimia 55 ya raia wa Marekani hawakubaliani na siasa za chuki na uhasama za serikali ya nchi hiyo dhidi ya Iran, asilimia 19 wameunga mkono na 26 hawakutoa maoni kuhusu suala hilo.
Tangu alipochukua madaraka ya nchi, Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akiishambulia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kutoa tuhuma za aina mbalimbali dhidi ya nchi hiyo. Vilevile amefanya jitihada kubwa za kutaka kuvunjwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na ametishia kuwa Washington itajiondoa katika makubaliano hayo yaliyopasishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa iwapo hayatafanyiwa mabadiliko.
chanzo:parstoday.

Comments