Ripoti zinasema Rais Joseph Kabila hakuwa ndani ya nyumba hiyo wakati iliposhambuliwa na waasi wa Mai Mai.
Shambulizi hilo la waasi limekabiliwa na mapambano makali ya jeshi la serikali lililofanikiwa kuwafurusha wapiganaji hao.
Shambulizi hilo ambalo ni pili dhidi ya nyumba ya Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika kipindi cha miezi mitatu ya hivi karibuni ni kielelezo cha kuzorota hali ya usalama kulikosababishwa na hatua ya Joseph Kabila kukataa kuachia madaraka baada ya kumalizika muhula wake wa utawala mwaka 2016.
Nyumba nyingine ya Rais Joseph Kabila ilishambuliwa na kuchomwa moto katika jimbo la Kivu Kaskazini Disemba mwaka jana.
Polisi mmoja aliuawa katika shambulizi hilo.
chanzo:parstoday.
Comments