
Katika hotuba yake aliyoitoa akiwa New
Hampshire,wauzaji wa dawa za kulevya wamesababisha vifo vya maelfu ya
watu, lakini cha ajabu baada ya kuhukumiwa kufungwa wanakaa muda mfupi
tu gerezani jambo ambalo anasema haliridhishwi nalo.
Ameongeza kuwa tatizo hili linaweza kuondolewa kwa kutumia akili na kuwa imara pamoja na kutenga fedha.
"Mwezi
oktoba tulitangaza tatizo hili kama janga la dharula kiafya ambalo
limedumu kwa muda mrefu tangu kipindi kilichopita.Tumelifanyia kazi na
bunge kuhakikisha tunatenga kiasi cha dola billion sita katika bajeti
mpya yam waka 2018/2019 ili kukabiliana na tatizo la dawa za
kulevya,ambapo tutakuwa tumetenga kiasi kikubwa cha fedha kuwahi kutokea
dhidi ya tatizo hili'.
Hata hivyo Rais Trump ameelezea mikakati iliyowekwa tayari katika kukabilianba na dawa za kulevya hadi sasa.
"Kwanza
kabisa tunapunguza kiwango uhitaji wa dawa hizo,kuhakikisha tunapunguza
idadi ya watu wanaojiingiza na hatimaye kutekewa na matumizi ya dawa za
kulevya,ni muhimu sana.
Hiyo inahusisha serikali kutoa fedha kwaajili ya
miradi isiyo jihusisha na masuala ya dawa za kupunguza maumivu,na
kuhamasisha matumizi ya dawa za kuondoa maumivu zisizo na madhara.Na ni
jambo lililo ndani ya uwezo wetu.
Lakini pia tunatoa ushauri,na idara
yetu ya inaliangalia suala hili kwa makini ikiwemo kuchukua hatua za
kisheria,na tutalisimamia katika hatua ya kiserikali''.
Rais Trump
ameahidi kujenga taifa huru katika masuala ya matumizi ya dawa za
kulevya kwa kizazi kijacho na kuhakikisha hakuna mazingira
yatakayosababisha watu kujitumbukiza katika matumizi ya kulevya.
chanzo:Bbc.
Comments