Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo amewataka
Watanzania kutumia vizuri fursa za masoko ya filamu kwaajili ya
kujiingizia kipato kwasababu Tanzania ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa
filamu Africa ikitanguliwa na Nigeria.
Akiongea
kwenye kikao na wadau wa filamu mkoani Shinyanga Bi. Fissoo amesema ni
lazima waigizaji watumie fursa zinazotengenezwa na Wizara ya Habari,
Utamaduni Sanaa na Michezo kwenye eneo la masoko ya filamu.
''Tunapozungumzia
filamu Tanzania ni ya pili baada ya Nigeria, na ukizungumzia Tanzania
pia Shinyanga ipo ndani yake kwahiyo hii ni fursa kwenu ambapo bodi ya
filamu na Wizara zinashirikiana kuhakikisha kazi za sanaa zinapata
masoko'', amesema.
Aidha
Katibu Mtendaji huyo wa bodi ameweka wazi kuwa Bodi hiyo imekuwa
ikifuatilia kila hatua ya wasanii ndio mana siku za hivi karibuni
ilimlipia tiketi ya ndege msanii mkongwe wa filamu Monalisa kwenda
kwenye sherehe za Tuzo huko nchini Ghana.
Monalisa
alichaguliwa kuwania tuzo ya mwigizaji bora wa kike Afrika kwenye tuzo
za The African Prestigious Awards zinazotolewa nchini Ghana. Msanii
mwingine ni Vicent Kigosi maarufu Ray ambaye naye alikuwa anawania
kipengele cha mwigizaji bora wa kiume.
chanzo:Mpekuzi.
Comments