
Alisema uchangamfu walionao baada ya uchaguzi lazima wauoneshe wakati
wa uchaguzi na watembee kifua mbele bila ya waoga wala wasiwasiwowote,
na kuhakikisha chama kinashinda.
Mjumbe huyo wa Kamati kuu ya CCM taifa, alieleza hayo jana Tawi la
CCM Ole wilaya ya Chakechake kisiwani humo, mara baada ya kuweka jiwe la
msingi la tawi hilo, ikiwa ni sehemu ya zaira yake ya siku tatukisiwani Pemba.
Alisema ndani ya CCM wapo waliokuwa hawana hamasa na kujinywezwa na
kuonekana kama CCM haipo kwenye jimbo la Ole na maeneo mengine kisiwani
Pemba, na kusahau kuwa wao taifa kubwa.
Alisema wanaccm wamekuwa waoga na kuogopa kung’ariwa na wapinzani na
kisha viapo wanavyokula vya kukulinda chama havina ukweli na nia thabiti
ndani yake.
Alisema, lazima vijana wa CCM wajenge ujasiri na uthubutu wa kweli na
kujiamini katika kukilinda chama na kuongeza idadi ya wanachama wapya
kila siku.
“Nyinyi ndio wale wanaccm mnaowatenga mwenzenu kwa sababu ya
kuzungumza na mtu anaefikiriwa kuwa ni cha cha upinzani, jamani siasa
hizo zimekwisha,”alisema.’
Katika hatua nyengine Mjumbe huyo wa Kamati kuu ya CCM taifa, alisema
lazima matawi ya CCM yatumike katika kuongeza idadi ya wanachama wapya
ili CCM kiendelee kushika hatamu.
Kuhusu wanaccm wanawake, Samia aliwataka kutekeleza kwa vitendo
nyimbo za umoja na mshikamano wanazoziimba, na sio kusema kwa mdomo
pekee bali iwe na kwa vitendo.
Alieleza kuwa, nyimbo kama ‘vigumu kutoka madarakani au tutaipigania
kw anguvu zatu zote’ alisema lazima wajipange vyema kivitendo na
kuhakikisha wanajitathimini na kama hawakubadilika wanaweza kutolewamadarakani.
Kuhusu ujenzi wa tawi hilo la CCM Ole, alisema anatamani limazike
mwishoni mwa mwaka huu ili liwezea kutumika kwa ajili ya matayarisho ya
uchaguzi mkuu wa 2020.
Alisema na yeye atahakikisha anafikisha mchango wake kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa tawi hilo, ili likamilike kwa wakati.
Akisoma risala ya ujenzi wa tawi hilo, Katib wa jimbo la Ole Yakoub
Khalfan, alisema hadi kufikia hatua ya ujenzi huo, shilingi milion 7.6
zimeshatumika ambapo nguvu za wanaccm wenyewe ni shilingi milion 1pamoja na mchango wa Mwakilishi wa jimbi hilo.
Alieleza kuwa, ili kuukamilisha ujenzi huo, hadi kuweza kutumika
shilingi milion 9.5 zinahitajika ambapo wanakusudia hadi mwishoni mwa
mwaka huu liwe limshakamilika.
Mjumbe huyo wa Kamati kuu ya CCM taifa amemaliza ziara yake ya siku
tatu kisiwani Pemba, ambapo alitembelea hospitali ya Abdulla mzee
Mkoani, uwekaji wa mawe ya msingi tawi la CCM Chumbageni, Ole, Ukunjwi,
skuli ya Micheweni, ujenzi wa nyumba za Polisi pamoja na skuli ya Ali
Khamis camp.
chanzo: zanzibar24
Comments