Rais John Magufuli amewataka maaskofu badala ya kuhubiri mambo mengine, wahubiri kuhusu ujenzi wa viwanda vya dawa nchini ili Tanzania isinunue dawa nje ya nchi.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Machi 26, 2018 katika hafla fupi ya ugawaji wa magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa ajili ya kusambaza dawa maeneo mbalimbali nchini inayofanyika eneo la Keko, jijini Dar es Salaam.
Amesema kununua dawa nje ya nchi kunasababisha nchi kupoteza Sh500bilioni.
“Asilimia 94 ya dawa zinanunuliwa nje ya nchi, ni asilimia sita tu ya dawa zinanunuliwa ndani,” amesema.
Amesema Rais Magufuli na kuwapongeza MSD kwa kufanya kazi nzuri na ya kizalendo.
Amesema kupatikana kwa magari hayo kumeifanya MSD kuwa na magari 213 kutoka magari 32 waliyokuwa nayo awali.
chanzo:Mpekuzi.
Comments