Rais
John Magufuli amewatajia wafanyabishara nchini mambo mawili muhimu
akiwataka kutumia fursa za masoko ya ndani ili kukuza ajira na kupunguza
uagizaji wa bidhaa kutoka nje.
Akizungumza
jana Jumatatu Machi 19, 2018 katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la
Biashara Ikulu Dar es Salaam, Dk Magufuli alisema mfanyabiashara yeyote
atakayekutana na vikwazo katika uwekezaji huo atoe taarifa mapema na
atachukua hatua kwa mteule wake aliyehusika.
Alitoa mfano wa fursa ya kuzalisha sare za wanafunzi na majeshi nchini.
“Tukisema
kwa mfano sare zote za wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi la saba,
kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita zizalishwe na viwanda vyetu vya
ndani au tukaanza kuzalisha viatu vya Jeshi, tutashindwa nini,”alisema Rais Magufuli.
Alisema Kiwanda cha Mwatex kitakapoanza kuzalisha sare hizo za wanafunzi, itasaidia kulinda soko la ndani, kuongeza uzalishaji wa zao la pamba na kukuza ajira kwa wakulima.
“Niwaambe
Watanzania wenzangu tuwe wazalendo, tukifanya hivyo tutakuwa tumejibu
hoja nyingi kwa wakati mmoja, atakayewakwamisha mniambie, mie si ndio
mwenyekiti wenu? Ili kusudi nimwambie na yeye akajaribu kufanya
biashara,”alisema.
chanzo:Mpekuzi.
Comments