Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amefunguka
na kuzungumzia suala la maandamano na kusema atashughulika na watu ambao
wataandamana ili wakawasilimulie wale watu ambao wamewatuma.
Rais
Magufuli amesema hayo leo Machi 9, 2018 wakati akizindua tawi la benki
ya CRDB Chato na kusema kuwa wapo watu ambao wanataka kuona amani ya
nchi hii inavurugika jambo ambalo yeye hawezi kukubali kwa kuwa alihapa
kulinda Katiba ya nchi.
"Wapo
watu wameshindwa kufanya siasa za kweli wangependa kila siku tuwe
barabarani tunaandamana, watu wao wanahamia huku wao wanataka wabaki
wanaandamana kule
"Nimeshasema
ngoja waandamane wataniona, kama kuna baba zao wanawatuma basi
watakwenda kuwasilimulia vizuri, niliapa kwa Katiba kwamba nchi hii
lazima iwe ya amani na tunataka tujenge uchumi wa kweli ili Watanzania
watajirike na hali ya Watanzania imeanza kwenda vizuri
"Mwanzo
ni mgumu lakini nataka niwaambie watanzania tupo kwenye wakati mzuri
tuvumiliane ili tufike sehemu Tanzania iwe nchi ya asali" alisema
Magufuli.
chanzo:Mpekuzi.
Comments