Putin: Damascus haina silaha za kemikali; magaidi ndio wanaotumia silaha hizo huko Syria.

Putin: Damascus haina silaha za kemikali; magaidi ndio wanaotumia silaha hizo huko SyriaAkizungumza katika mahojiano na televisheni ya NBC, Rais wa Russia ameeleza kuwa madai yanayotolewa na Marekani kwamba serikali ya Syria inatumia silaha za kemikali ni ya uwongo na kwamba magaidi ndio wanaotumia silaha hizo huko Syria.

Rais Vladimir Putin ameongeza kuwa magaidi wanafanya kila wawezalo kuinasibisha serikali ya Syria na mashambulizi yao ya kemikali. 
Rais wa Russia amebainisha kuwa magaidi wanatekeleza hatua hiyo ili kuwaunganisha mamluki wao kukabiliana na serikali ya Syria. 
Rais Putin amesisitiza kuwa Russia inataka kufanyika uchunguzi kamili kuhusu suala hilo. 
Marekani na nchi waitifaki wake hadi sasa zimejaribu marakadhaa kuyanasibisha mashambulizi hayo ya kemikali na serikali ya Syria; tuhuma ambazo zimekanushwa vikali mara kadhaa na Damascus. 
Ripoti rasmi zinaonyesha kuwa magaidi wametumia silaha za kemikali mara kadhaa huko Iraq na Syria. 
Weledi wengi wa mambo wanaamini kuwa kitendo cha kuituhumu serikali ya Syria kwamba imetumia silaha za kemikali nchini humo ni njama zenye lengo la kuzipotosha fikra za waliowengi na uhakika wa mambo kufuatia ushindi wa hivi karibuni wa jeshi la Syria dhidi ya magaidi nchini humo. 
Hivi karibuni pia Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ilitangaza  Marekani na waitifaki wake wanaituhumu serikali ya Syria kuwa imetumia silaha za kemikali ili kuwanasuru magaidi. 
 chanzo:parstoday.

Comments