PSG yanusa ubingwa Ufaransa, Napoli yaishika pabaya Juve.


PARIS St-Germain imekaribia taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa ‘Ligue 1’ kufuatia ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Nice.

Beki mkongwe, Dani Alves ndiye aliyeibuka shujaa wa PSG baada ya kufunga goli la ushindi kwenye dakika ya 82 huku Angel di Maria akifunga kunako dakika ya 21.

Lakini, Nice ilikuwa ya kwanza kuziona nyavu za PGS kwenye dakika ya 17 kupitia kwa Allan Saint-Maximin aliyemalizia kazi nzuri ya Alassane Plea.

Mshambuliaji, Mario Balotelli aligongesha mti mara mbili kabla ya Alves kujitwika krosi ya Adrien Rabiot na kuihakikishia ushindi PSG.

PSG alishinda taji hili katika misimu minne mfululizo kabla ya kumaliza nafasi ya pili nyuma ya Monaco msimu wa 2016-17.

Hata hivyo, mafanikio haya ya hivi karibuni yalikuwa ya kushinda ‘Ligue 1 kwa mara ya tisa mfululizo na inawaacha pointi 17 safi mbele ya Monaco ambayo imebakisha mechi nane msimu huu. waliosalia kucheza msimu huu.

Nice ambayo ilishika nafasi ya tatu msimu uliopita,hivi sasa ipo nafasi ya nane.

Nayo Napoli iliendelea kuifukuza kimya kimya Juventus baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Genoa,katika mchezo wa Ligi wa Ligi Kuu ya Italia.

Beki, Raul Albiol,alifunga goli hilo pekee kwenye dakika ya 72 na kuifanya timu hiyo kukaa nyuma ya Juventus kwa tofauti ya pointi mbili.

Kikosi cha Maurizio Sarri,kilitumia fursa ya Juve kulazimishwa 0-0 na vibonde SPAL.

Beki huyo wa zamani wa Real Madrid, Albiol, alifunga goli hilo kwa kichwa kufuatia kona ya Jose Callejon,ikiwa la kwanza kwake tokea Januari 2016.(AFP).

Comments