
Mtandao huu umeshuhuidia
maendeleo ya uwanja huo yanavyoendelea ambapo kwasasa mafundi hao
wanatandaza nyasi bandia huku zoezi hilo likitarajiwa kukamilika muda
mchache.
Tayari uwanja huo umeshawekwa Taa ambazo zitasaidia kuchezwa michezo hadi usiku huku baadhi ya vifaa vyengine vinazidi kutoa sura mpya ya kukamilika kwa ujenzi huo kadri ya siku zinavyokwenda.
Ujenzi wa uwanja huo unafuatia msaada mkubwa ulioidhinishwa na
Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar katika azma ya kuimarisha uhusiano wa muda mrefu wa pande hizo
mbili ukizingatia heshima uliopewa Uwanja huo wa kuitwa jina la Muasisi
wa Taifa la China Hayati Mao Tse Tung.
Uwanja huo utakuwa na Viwanja viwili vya mpira wa miguu na chengine
cha Mpira wa Kikapu, Mpira wa Mikono, Mpira wa Pete na na michezo
mengine ya ndani kama vile Mpira wa Meza pamoja na sehemu ya kufanyia
mazoezi ya kuinua vitu vizito.
Katika Viwanja hivyo vya Mpira wa Miguu uwanja mmoja utakuwepo upande
wa Magharibi ambao utakuwa na Jukwaa moja litakalochukuwa Mashabiki
1500 waliokaa.
Uwanja mwengine wa mpira wa miguu utakuwepo upande wa Mashariki ambao
utakuwa na uwezo wa kuchukua Mashabiki waliokaa 900 katika jukwaa moja
ambalo litakuwepo katika Uwanja huo.
Uwanja huo utagharimu Shilingi Bilioni 12.5 kwa fedha za Tanzania
ambapo Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China itatoa Shilingi Bilioni 11.5
huku Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itachangia zaidi ya Shilingi
Bilioni 1 kati ya hizo Bilioni 12.5 ambazo watalipwa Wakandarasi wa
uwanja huo ambao ni Kampuni ya Zhengtar Group Company Limited ambayo ina
uzoefu mkubwa wa kujenga Viwanja wa Michezo.
Chanzo:Zanzibar24.
Comments