
1.Afisa Mipango Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Mipango’ au ‘Uchumi’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
2.Afisa Takwimu Daraja la II “Nafasi 2”
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Takwimu’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
3.Afisa Maendeleo ya Viwanda Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Uhandisi wa Viwanda’ au elimu inayolinagana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
4.Karani Mapato Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada ya ‘Uhasibu’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
5.Mlinzi Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amemaliza elimu ya Sekondari.
•Awe amepata mafunzo ya Ulinzi (Mgambo au JKU au JKT)
6.Muhudumu Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe na elimu ya Sekondari na kuhitimu mafunzo ya uhudumu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
7.Msaidizi Afisa Usafiri Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya ‘Usafiri’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
8.Afisa Biashara Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Biashara’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jinsi ya Kuomba:
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 – ZANZIBAR.
•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi
ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani
Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa
kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma
na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi
anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.
Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 05 Aprili, 2018 wakati wa saa za kazi.
Comments