
1.Karani Mapato Daraja la III “Nafasi 1” – Pemba.
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada ya Uhasibu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
2.Afisa Utumishi Msaidizi Daraja la III “Nafasi 1” – Pemba.
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Rasilimali Watu au Utawala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
3.Wahasibu Daraja la II “Nafasi 6” – Pemba.
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Uhasibu’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
4.Wasaidizi Wahasibu Daraja la III “Nafasi 6” – Pemba.
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya ‘Uhasibu’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
5.Wakaguzi wa Ndani Daraja la II “Nafasi 10” – Pemba.
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Uhasibu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
6.Wahakikimali Daraja la II “Nafasi 4” – Pemba.
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Ununuzi na Ugavi’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
7. Afisa Uhakikimali Msaidizi Daraja la III “Nafasi 2” – Pemba.
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya ‘Ununuzi na Ugavi’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jinsi ya Kuomba:
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 – ZANZIBAR.
•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi
ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani
Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa
kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma
na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuiainisha nafasi
ya kazi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.
Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 16 Machi, 2018 wakati wa saa za kazi.
CHANZO: zanzibar24.
Comments