Zahr Birawi, Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Kuvunja Mzingiro wa Ghaza amesema harakati yao inalenga kuufahamisha ulimwengu kuhusu mzingiro wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza kwa lengo la kuhitimisha mzingiro huo,
Tokea mwaka 2006, utawala wa Kizayuni wa Israel uliweka mzingiro wa nchi kavu, anga na baharini dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza. Katika mzingiro huo, Israel inazuia bidhaa muhimu kama vile, petroli, umeme, dawa, chakula na vifaa vya ujenzi kufika katika Ukanda wa Ghaza.
Birawi amesema mwaka huu meli kadhaa kutoka nchi kadhaa za Ulaya zitaelekea Ukanda wa Ghaza kwa lengo la kuvunja mzingiro wa Ghaza na kwamba wanaharakati muhimu wa kimatiafa watakuwa katika misafara hiyo.
Itakumbukwa kuwa mwaka 2010 askari wa Israel, walishambulia msafara wa baharini uliopewa jina la 'Uhuru wa Gaza' na ambao ulizijumuisha meli sita zilizokuwa zimebeba wanaharakati wa amani 663 kutoka nchi 37 za dunia.
Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa hali katika Ukanda wa Ghaza ni mbaya mno na eneo hilo liko katika ukingo wa kukabiliwa na maafa makubwa ya kibinadamu ambapo Wapalestina miloni moja na nusu wanakabiliwa na hatari ya kuangamia.
chanzo:parstoday.
Comments