Video
vixen maarufu kutoka nchini Kenya anayejulikana kama Tanasha Donna
Barbieri Oketch ‘Zahara Zahire’ ambaye alionekana kwenye video ya wimbo
wa Alikiba na Christian Bella ‘Nagharamia’ amekataa kuwa na uhusiano na
Alikiba.
Kwa
wiki sasa kumekuwa na taarifa zilizokuwa zinaenea mtandaoni ambazo
zinadai kuwa supastaa huyo wa Bongo fleva Alikiba anatarajia kufunga
ndoa hivi karibuni lakini tatizo likawa bibi harusi hajulikani ni nani.
Lakini
mara moja habari zilianza kuenea kuwa mrembo ambaye anatarajiwa kuolewa
na Alikiba ni mkenya anayeishi Moombasa na baadae kuja kusikika bibi
harusi ni Tanasha.
Tanasha
amejitokeza na kukataa kata kata taarifa hizo za kuolewa na Alikiba
wala kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi. Tanasha aliweka wazi ujumbe huo
kwenye ukurasa wake wa SnapChat ambapo aliandika;
Kwenye
ujumbe huo Tanasha ameelezea kuwa taarifa zinaoenea kwenye mitandao
Tanzania kuwa ana uhusiano na Alikiba ni za uongo na uzushi na kudai
aliwahi kutokea kwenye video yake moja tu ya wimbo wake lakini
hawajawahi kuwa wapenzi.
chanzo:Mpekuzi.
Comments