Mchungaji
mmoja kutoka Nigeria (39), Andrew Ejimadu wa kanisa la Christ Freedom
Ministries amezua gumzo mtandaoni baada ya ku-post picha zake katika
mtandao wa Facebook wakati wa kuabudu mitandaoni.
Nabii huyo ameshangaza maelfu ya watu baada ya kuonyesha picha za waumini wa kanisa lake wakibusu na kulamba viatu vyake akidai kuwa kwa kufanya hivyo watapata baraka na miujiza.
Nabii huyo aliweka picha hizo katika ukurasa wake na kuandika.“Nimebariki miguu yako, nimeosha nyayo zako.”
“Kitu
cha kwanza kesho asubuhi, ikiwa utaandika Amen na ushirikishe ujumbe
huu, kuna mtu atakupigia simu na miguu yako itakubeba hadi huko kuchukua
zawadi maalum. Watu wengi watakosa hilo, jaribu,” Andrew Ejimadu.
Mwaka
2016, Mchungaji Ejimadu alipamba vichwa vya habari na kushikiliwa na
polisi nchini Zambia yeye na kaka yake, Cleopasa Ejimadu kwa kosa la
kumbaka binti mdogo mwenye umri wa miaka 14 ambaye alikwenda kwenye
makazi yao kwa ajili ya uponyaji na kupata ushauri WA kiroho.
chanzo:Mpekuzi.
Comments