
Habari za uhakika zilizoifikia leo Machi 5, 2018, zinasema jana
alipofikishwa katika hospitali hiyo saa mbili usiku na madaktari
walimwekea mashine ya kumsaidia kupumua.
Taarifa za kulazwa kwa mwenyekiti huyo ambaye pia ni kiongozi wa
Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB) na Mbunge wa Hai zilianza kuzagaa leo
baada ya watu kumuona hospitalini hapo.
Katibu wa Chadema mkoa Kilimanjaro, Basil Lema alipoulizwa juu ya
kulazwa kwa kiongozi huyo alionekana kusita kuzungumza na kuhoji ni nani
aliyetoa taarifa hizo.
Hata hivyo amesema, “Ni kweli jana aliugua ghafla na
kupelekwa KCMC na madaktari walilazimika kumwekea Oksijeni ili ku
stabilize (kudhibiti) afya yake lakini baadaye waliondoa hiyo Oksijeni
baada ya afya yake kuimarika.
Lema alikataa kuingia kwa undani ugonjwa unaomsumbua kiongozi huyo
akisema suala hilo ni siri ya mgonjwa na daktari wake zaidi ya kufafanua
tu kuwa alipelekwa hospitalini hapo jana.
Habari zaidi zilizopatikana zilieleza kuwa asubuhi hii madaktari
bingwa wa hospitali hiyo walikuwa wakimchukua vipimo ili kubaini maradhi
yanayomsumbua.
Chanzo: Mwananchi na zanzibar24.
Comments