Msanii
wa muziki wa injili nchini Emmanuel Mbasha amefunguka katika ukurasa
wake wa instagram kwa kumuandikia barua ndefu aliyekuwa mke wake wa ndoa
Florah Mbasha kuhusu kumnyima mtoto wake wa kike waliezaa nae
walipokuwa wakikaa wote miaka ya nyuma.
Emanuel
Mbasha na Flora Mbasha walifunga ndoa kanisani na kuishi pamoja na hata
kufanya kazi zao za muziki wa injili pamoja lakini walikuja kuachana na
hata kupelekana mahakamani kwa makosa ya kubaka ambapo baada ya
upelelezi kukamilika ilikuja kuonekana kwamba Florah Mbasha alitunga
kesi hiyo na kumsingizia mume wake hivvyo Emanuel Mbasha alichukua
jukumu la kumtaliki mwanamke huyo.
Lakini
Emanuel Mbasha anaonekana kuumia kukaaa mbali na mtoto wake wa kike
walimpata na mzazi mwenzie huyo ambae alipewa mamlaka ya kukaa na mtoto
huyo na mahakama kutokana na umri wa mtoto, Mbasha anasema kuwa pamoja
na kwamba mahakama iliamuru mtoto kukaa na mama yake na yeye kuruhusiwa
kumuona kwa muda tu lakini hata muda kidogo amekuwa akinyimwa na mzazi
mwenzie huyo.
"Happy
women’s day, ila ulinizalia mtoto mzuri mno nakushukuru sana,nimemmiss
sana lizy unipage basi hata mtoto , unaninyima hata kumuona , karibia
mwaka wa 2 unaelekea wa 3 sasa sijawahi kumuona mtoto daah mie babake tu
ila naomba siku moja moja nifurahie maisha , aah nakuomba nimuone
mwanangu lizy,najua hata mtoto amenimiss sana maana najua ameonoka
kwangu akiwa mkubwa na nimemlea tamgu akiwa mtoto , atakuwa anshindwa tu
kusema ila amenikumbuka sana.mahakama iliamua mtoto akae na mama ila
niwe namuona mtoto ,sasa unapingana na mahakama…. sitaki povu hapa
naongea na mzazi mwenzangu maana naona njia za kawaida zimeshinikana
sasa inabidi nikuombe insta."
Mbasha
anAsema kuwa ameamua kutuma ujumbe huo kwa Florah Mbasha ambae kwa sasa
ameshaolewa na mwanaume mwingine kupitia instagram kwa sababu hakuna
njia nyingine wanaweza kuwasiliana zaidi ya hiyo,
chanzo:Mpekuzi.
Comments