MAKAMU
Mwenyekiti wa CCM Bara, Philipo Mangula amewataka Watanzania kujenga na
kuilinda amani nchini na kushangazwa na viongozi wa dini wanaobariki
chuki kuwa wanamkosea Mungu.
Pia
aliwaonya wanasiasa wanaochochea chuki na kusababisha vurugu na
kuwashauri waache kwa kuwa siasa ni uvumilivu na kuvumiliana.
Mangula
alitoa kauli hiyo juzi mjini Musoma alipozungumza na viongozi na wana
wana chama wa CCM kwenye ukumbi wa mikutano wa Chama mjini humo.
Alisema
kuwa turufu kubwa iliyobaki kwa CCM na watanzania ni amani iliyodumu
nchini kwa miaka dahari na hivyo wakati wote wazungumzie taratibu na
kutunza amani ya nchi ili kue[uka machafuko vurugu na migogoro
inayosababishwa na kuchochewa na wanasiasa.
“Siasa
ni kuvumiliana na uvumilivu ndiyo hujenga umoja.Wanasiasa wanapoleta
vurugu wajue wanaoumia ni watoto na wanawake na hivyo tuache chuki
tujenge amani ya nchi yetu bila kufanya hivyo hatuwezi kupata
maendeleo,”alisema Mangula na kuongeza kuwa;
“Nashangaa
na kushitushwa na viongozi wa dini wanapojiingiza na kubariki chuki,
wanamkosea Mungu. Machafuko yakishatokea hakuna atakayesalimika kwa
kusema mimi ni kiongozi wa dini."
Alieleza kuwa kazi ya serikali si kuwajengea nyumba bali mazingira mazuri wananchi ili wajijenge na kujifanyia maendeleo.
Makamu
Mwenyekiti huyo wa CCM bara alieleza zaidi kuwa yapo mabadiliko makubwa
ya maedeleo mkoani Mara na yote hayo yanafanyika kwa kuwa nchi ina
utulivu kwani bila amani ni vigumu kupata maendeleo na hivyo amani
kwanza taratibu na kanuni zifuatwe baadaye.
Alisisitiza
wanasiasa kuwa wanapochochea chuki na vurugu wanakuwa na passports
(hati za kusafiria) mikononi na yakichafuka wanaondoka na kuwaonya wana
CCM wasijiingize kwenye migogoro hasa vijana wa CCM wasijiingize humo.
Aidha,
Mangula aliwapongeza wabunge wa CCM mkoani Mara walio karibu na
wanaotekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM na ahadi kwa wananchi na wapiga
kura wao.
Awali
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Samuel Kiboye Namba Tatu alisema Mangula
ni miongoni mwa viongozi waadilifu waliobaki ndani ya CCM na Tanzania.
Alimpongeza
kwa kumsaidia Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais John Magufuli na kuiwezesha
CCM kurudisha heshima kwa wananchi na akawataka wana CCM kumuombea
maisha marefu.
“Nakupongeza
kwa kumsaidia Rais Magufuli na sisi huku chini hatutamvumilia mtu
yeyote asiye na nidhamu wala maadili.Wabunge wa CCM nao wamejitahidi
kutekeleza ilani ya Chama hasa mbunge wa Musoma Mjini jimbo ambalo ni
gumu kisiasa,”alisema Namba Tatu.
Kwa
mujibu wa habari za ndani ya chama hicho, Mangula atakuwa na ziara ya
siku tatu katika wilaya za Tarime, Serengeti na Bunda ambako atafanya
vikao na viongozi wa serikali na jumuiya za CCM.
Jumanne
na Jumatano atakuwa Tarime, Alhamisi na Ijumaa atakuwa Serengeti kabla
ya kuhitimisha ziara yake jumapili wilayani Bunda.
chanzo:Mpekuzi.
Comments