
Majimaji ambayo kabla ya mchezo wake wa jana Alhamisi dhidi ya Ndanda
FC ilikuwa inaburuza mkia ikiwa na pointi 15 katika michezo 20,
inahitaji kupambana vilivyo kuhakikisha haiwi kwenye nafasi mbili za
timu ambazo zitashuka daraja mwishoni mwa msimu huu.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Ofisa Habari wa Majimaji, Onesmo Ndunguru alisema:
“Kiukweli
tunaweza kusema tuna hali mbaya na Mungu pekee ndiye anayeweza kutuokoa
na janga la kushuka daraja, hivi sasa tunazipigia hesabu mechi zetu
hizi za hivi karibuni ambapo tunahitaji kushinda zote ili kutoka huku
chini.
“Haitakuwa rahisi, tuna kazi kubwa ya kufanya ya kupata
ushindi mechi hizo ili tuwe sehemu salama, Jumapili tuna mechi dhidi ya
Lipuli kwenye uwanja wetu wa nyumbani, hatutakuwa tayari kuona
tunashindwa kupata matokeo mazuri nyumbani.”
chanzo: zanzibar24.
Comments