
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed amesema kumekuwa na malalamiko mengi kwa wananchi kutorizika na utendaji wa wizara hiyo , hivyo ili kuondoa malalamiko hayo lazima watendaji wawajibike kikamilifu bila ya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Amesema Serikali inatambua kuwepo kwa upungufu wa madaktari lakini watendaji wasichukue kigezo hicho cha kuwacha kuwajibika katika majukumu yao na wakumbuke kuwa kazi ya kuwahudumia wananchi ni ya mashirikiano.
Hata hivyo Hamad amesema mbali na hayo pia lipo tatizo kwa baadhi ya watendaji kuuza bidhaa za serikali ikiwemo dawa jambo ambalo nikinyume kisheria kwani dawa hizo serikali inazitoa bure kwa wananchi hivyo nivizuri kwa kila mwenye zamana kusimamia zamana yake na kuwacha tabia hizo mbaya zinazoichafua Wizara ya Afya.
chanzo:Zanzibar24
Comments