Leo ni Jumatatu tarehe 5 Machi, 2018.

Jumatatu tarehe 5 Machi, 2018Leo ni Jumatatu tarehe 16 Jamadithani 1439 Hijria mwafaka na tarehe 5 Machi 2018.

Miaka 1018 iliyopita katika siku kama ya leo, alifariki dunia Ibn Darraj Qastalli mshairi na mwandishi mwashuhuri wa Andalusia. 
Ibn Darraj alizaliwa mwaka 347 Hijiria na alikuwa miongoni mwa washairi wakubwa wa Andalusia huko kusini mwa Uhispania ya leo. Pia alikuwa na nafasi muhimu katika kukuza mashairi ya Kiarabu mwishoni mwa karne ya 4 na mwanzoni mwa karne ya 5 Hijiria. 
Ibn Darraj ndiye aliyeleta mtindo mpya wa mashairi ya Kiarabu huko Andalusia na mashairi yake mbali na kuwa na thamani ya kifasihi na kisanaa pia yanahesabiwa kuwa chanzo cha kuaminika kinachoonyesha matukio ya wakati huo ya Uhispania. 
Siku kama ya leo miaka 191 iliyopita, sawa na tarehe 5 Machi 1827 alifariki dunia Alessandro Volta, mtaalamu wa fizikia wa Italia akiwa na umri wa miaka 83. 
Sambamba na kufundisha katika chuo kikuu, Volta alikuwa akifanya uhakiki na alifanikiwa kutengeneza chombo cha kupimia kiwango cha umeme, Electrometre. 
Miaka191 iliyopita katika siku kama ya leo, alifariki dunia Pierre Laplace mwanahisabati mashuhuri wa kifaransa.
 Alizaliwa mwaka 1749 na baada ya kuhitimu masomo yake alijishughulisha na kufundisha  hisabati. 
Laplace alitumia sehemu kubwa ya umri wake kutwalii na kufanya uhakiki kuhusiana na elimu za nujumu na hisabati.
Tarehe 5 Machi miaka 65 iliyopita alifariki dunia Joseph Stalin, kiongozi na dikteta wa Urusi ya zamani. 
Stalin alizaliwa mwaka 1879 nchini Georgia na alijiunga na mrengo wa kikomunisti baada ya kusoma fikra za mrengo huo. 
Joseph Stalin alipelekwa uhamishoni huko Siberia mwaka 1913 kutokana na harakati zake za kisiasa dhidi ya serikali ya wakati huo ya Urusi. 
Stalin alibakia huko hadi baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Urusi mwaka 1917. 
Alipata vyeo vya ngazi za juu wakati wa uongozi wa Lenin na alishika uongozi wa nchi hiyo akiwa pamoja na wanasiasa wengine mashuhuri baada ya kufariki dunia Lenin.
 Mwaka 1927 Stalin aliwafutilia mbali wapinzani wake ndani ya chama na kuwa kiongozi asiye na mpinzani katika Chama cha Kikomunisti. Joseph Stalin aliendelea kuwafuta na kuwaangamiza bila ya huruma wapinzani wake ndani na nje ya chama hicho.
Na siku kama ya leo miaka miwili iliyopita alifariki dunia mbunifu wa E-mail yaani baruapepe, Ray Tomlinson. 
Tomlinson ambaye mwaka 1971 alikuwa akifanya kazi katika kampuni moja ya uhakiki kama mhandisi huko Boston nchini Marekani alianzisha mfumo wa awali wa E-mail katika mtandao wa Arpanet yaani nakala ya kwanza na intaneti. 
Mtaalamu huyo kwa hakika alituma baruapepe ya kwanza kabisa kwa mtindo wa kisasa. 
Ray Tomlinson alifariki dunia katika tarehe aliyozaliwa akiwa na umri wa miaka 75 kutokana na ugonjwa wa kiharusi.  
 Hii nikwahisani ya parstoday.

Comments