Jeshi
la Polisi mkoani Mwanza limewaonya baadhi ya watumiaji wa mitandao ya
kijamii wanaotumia vibaya mitandao hiyo kufanya uhalifu ikiwemo
kuhamasisha maandamano haramu
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Naibu Kamishina Ahmed Msangi
ametoa onyo hilo hii jana wakati akizungumza na askari waliokuwa
kwenye mazoezi mbalimbali yaliyofanyika katika uwanja wa polisi Mabatini
Jijini Mwanza.
RPC Ahmed Msangi alisema;
"Kuna watu wanapeana vihabari vya kwenye mitandao ya kijamii wafanye
uhalifu na uhalifu wenyewe ni wa kufanya maandamano au mkutano usiokuwa
na taarifa na kiukweli imepigwa marufuku"
Aidha,
RPC Msangi wamewataka Polisi kufanya uchunguzi ili kuwabaini
wanaoshinikiza hayo na kisha kuwahoji na kujua nia yao ya kutaka kufanya
hivyo ni ipi
Baadhi ya askari walioshiriki mazoezi hayo wameeleza kwamba yanawasaidia kuwa imara wakati wote na hivyo kutimiza vyema majukumu yao.
Baadhi ya askari walioshiriki mazoezi hayo wameeleza kwamba yanawasaidia kuwa imara wakati wote na hivyo kutimiza vyema majukumu yao.
chanzo:Mpekuzi.
Comments