India: Raia wetu 39 waliotekwa na Daesh nchini Iraq, waliuawa na magaidi hao.

India: Raia wetu 39 waliotekwa na Daesh nchini Iraq, waliuawa na magaidi haoWaziri wa Mambo ya Nje wa India amethibitisha habari ya kuuawa raia 39 wa nchi hiyo waliotekwa na wanachama wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) nchini Iraq miaka michache iliyopita.

Sushma Swaraj ameyasema hayo Jumatano ya jana na kuongeza kuwa, tayari amemtaka VK Singh, Mshauri wa Waziri wa Mambo ya Nje wa India kwenda Iraq kwa ajili ya kufanya taratibu za kurejeshwa mabaki ya miili ya watu hao. Hii ni katika hali ambayo mwaka uliopita 2017, Sushma Swaraj alijiepusha kuthibitisha iwapo raia hao wa India walikuwa tayari wameuawa na magaidi hao au la.
Inaelezwa kuwa, raia hao wa India walikuwa wakijishughulisha na kazi ya ujenzi wa hospitali moja mjini Mosul, ambapo baada ya mji huo kudhibitiwa na magaidi hao wa Kiwahabi mwaka 2014 walihamishiwa katika jela ya kaskazini magharibi mwa mji huo. 
Tangu kipindi hicho, serikali ya India ilikuwa ikifanya mawasiliano na serikali ya Iraq kwa lengo la kuwapata raia wake hao, ingawa hata hivyo juhudi hizo hazikuzaa matunda. 
Mabaki ya miili ya watu hao ilipatikana hivi karibuni ndani ya kaburi la umati katika kijiji cha eneo la kaskazini magharibi mwa mji wa Mosul, ambapo baada ya kufanyiwa uchunguzi, iligundulika kuwa ni ya raia hao wa India.
Baada ya mji wa Mosul kudhibitiwa na wanachama wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) ambao wanaungwa mkono na Marekani na nchi kadhaa za Magharibi, Saudia, Imarati, Israel na baadhi ya nchi za eneo, walifanya jinai kubwa dhidi ya binaadamu. 
Hata hivyo kusimama imara jeshi la Iraq kwa kushirikiana na jeshi la kujitolea la wananchi la Hashdu sh-Sha'abi na kwa msaada mkubwa wa washauri wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kulifanikisha kuwasambaratisha magaidi hao mjini Mosul na maeneo mengine ya Iraq.
chanzo:parstoday.

Comments