“Habari
Grace. Ninaitwa Ninah, ningependa katika simulizi unazotuma fesibuku,
nikupe na wosia wa kaka yangu marehemu, uwaandikie watu. Kabla hajafa
aliniomba sana niwambie watu wengi kadiri niwezavyo kile alichotaka
wajue. Akaniachia barua ndefu sana aliyoiandika mwenyewe”
Nilisoma
ujumbe huo nikastuka na kutamani kujua huo wosia wa marehemu aliotaka
uwafikie watu unahusu nini. Nilimpa anuani yangu ya barua pepe na
kumuomba aniandikie huo wosia humo, nijue kama kweli ungefaa kuwafikia
watu kama ambavyo marehemu alidai.
Nirudi
nyuma kidogo, Kuna mdogo wangu yuko katika kundi moja la fesibuku, la
wasichana na wanawake, amekuwa akinisimulia visa kadha wa kadha
vinavyowatokea wadada wengi walio kwenye ndoa.
Mambo
mengi ambayo huwa hunisimulia hunifanya nijue kumbe kweli UKIMWI bado
upo na unaua. Kuna kisa fulani aliniambia miezi kadhaa iliyopita,
kikanifanya nitamani kama watu wengi zaidi wangeelewa uhalisia wa huu
ugonjwa na jinsi unavyowamaliza wengi mpaka leo hii, hata wale
wasiotegemea.
Mbaya
zaidi kwa sasa ambapo kumekuwa na dawa za kuongeza kinga, wagonjwa
wengi wa UKIMWI hawajulikani kwa kuonekana kwa macho, na huo umekuwa
mtego kwa watu wengi.
Kuna
binti mmoja, nitampa jina la Vero, kwenye hilo kundi ana ndoa ya miaka
mitatu na wana mtoto mmoja, aliwahi kufuma jumbe za mapenzi kwenye simu
ya mume wake, mwanaume akawa akijitetea na kuomba msamaha, binti
akasamehe.
Siku
moja binti aliamua kufuatilia namba, alipofuma tena ujumbe wa mapenzi
kwa mume wake, akaja kugundua kumbe ni ya jirani yao, cha kumshangaza
zaidi huyo jirani yao ni kijana wa kiume.
Binti
akachanganyikiwa ndipo akaamua kuomba ushauri kwenye hilo kundi, pasipo
kujitaja jina lake, watu wakamshauri asamehe, asimfuatilie mwanaume,
wengine wakashauri aachane naye, na kuna waliomshauri akapime na
akikutwa salama basi amuache.
Sasa
akiwa anafikiria nini cha kufanya, siku mbili baadaye akiwa nyumbani
kwake, alitembelewa na jirani yake mwingine nitamuita Siwema. Katika
maongezi yule mwanamke Siwema, bila kujua chochote akaanza kuelezea kuwa
yule kijana jirani ambaye Vero aligundua kwamba ana mahusiano na mumewe
ni shoga na ni muathirika.
Siwema
aliongea kwa malalamiko kuwa kuna mtoto wa dada yake (naye ni wa kiume)
alikuja kuishi kwake kwa muda wa miezi mitatu akiwa likizo ndefu ya
chuo kikuu, kumbe walianzisha mahusiano na yule mvulana. Sasa anadai
siku kadhaa zilizopita amegundulika ameathirika, amechanganyikiwa sana
kijana pamoja na mama yake.
Siwema
alisema alishasikia tetesi hapo nyuma kuwa yule kijana ameathirika, ila
hakutilia mkazo sana, mpaka alipogundua amemuambukiza huyo mtoto wa
dada yake, kwani kijana baada ya kupimwa na kukutwa na UKIMWI alimueleza
mama yake ukweli kuhusu ni wapi anahisi ameutoa.
Akielezea
tena Vero kupitia kwa kiongozi (admini) wa hilo kundi, alisema, “Nikiwa
bado nawaza kuhusiana na ushauri wenu, nilikuja kugundua kuwa yule
kijana anayetembea na mume wangu ni kweli ni shoga na ameathirika.
imeandaliwa na Mpekuzi.
Comments