Wakili
wa kujitegemea, Fatma Karume amejitosa kumrithi Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu kwa kugombea urais wa Chama cha Mawakili wa
Tanganyika (TLS), utakaofanyika Aprili 14, mwaka huu.
Lissu,
ambaye aliteuliwa kugombea nafasi hiyo lakini ameshindwa kukidhi
matakwa ya kamati kutokana na fomu ya uteuzi iliyowasilishwa kwa
sekretarieti hiyo.
Kwa
mujibu wa sheria mpya, Lissu hataweza kugombea tena nafasi hiyo kwani
kifungu cha nane cha sheria hiyo, kinamzuia mtu ambaye ni kiongozi wa
chama chochote cha siasa, kuongoza chama hicho.
Katika
kinyang’anyiro hicho, Fatma atachuana na Godwin Mwapongo, Godfrey
Wasonga na Godwin Ngwilimi huku nafasi ya umakamu wa rais ikiwa na
mgombea pekee, Rugemeleza Nshalla na Mweka Hazina akiwa Sadock Magai.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uteuzi wa chama hicho, Dk.
Kibuta Ongwamuhana, uchaguzi wa rais utatanguliwa na viongozi wa kanda
utakaofanyika kila mkoa kuanzia Machi 27, mwaka huu.
Wakizungumzia
uchaguzi huo baadhi ya mawakili wamesema wanamtabiria Fatma ushindi wa
kishindo kutokana na kuwa na kariba inayofanana na Lissu.
“Fatma
atashinda kwa sababu anapenda mtu mwenye ‘tension’ na ni mtu mwenye
kujiamini anaweza akaitetemesha serikali na wanasheria wanapenda hivyo,”
amesema mawakili wa kujitegemea ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Wakili
mwingine alisema ingawa sheria hiyo inamkataza Lissu kugombea ambapo
walipanga kumchagua tena mwaka huu lakini Fatma anaweza kuziba pengo la
Lissu.
chanzo:Mpekuzi.
Comments