Kufuatia
baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii kuhusisha upunguaji wa mauzo
ya Soko la Hisa la Dar es Salaam-DSE na hali ya uchumi, Afisa Mtendaji
Mkuu wa Soko hilo Moremi Marwa ametoa ufafanuzi wa muenendo wa soko
hilo.
Amesema
kupungua huko ni hali ya kawaida katika soko kunakotokana na wawekezaji
kupendelea kubadili uwekezaji kutoka kwenye hisa kwenda kwenye hati
fungani, na kwamba hali hiyo ikitokea mauzo ya hisa hushuka wakati ya
hati fungani yakipanda.
Huku
akirejea takwimu zinazoonyesha mwenendo wa soko katika kipindi cha robo
mwaka wa 2017 na 2018, amesema kuanzia Januari hadi Machi 10 mwaka huu
kulikuwa na miamala ya mauzo ya hisa zenye thamani ya jumla ya Sh.
bilioni 72 na mauzo ya hati fungani-Bonds yalikuwa na thamani ya bilioni
287 kwa bei ya kuuzia.
Ukilinganisha
na kipindi cha robo mwaka cha 2017 ambapo kulikuwa na miamala yenye
thamani ya sh. 75 na thamani ya bonds ilikuwa bilioni 229, na kwamba
mwaka huu mauzo ya bonds yalipanda kwa bilioni 58 hali iliyopelekea
kushuka kwa mauzo ya hisa.
“Tunaweza
kusema mwenendo ni kuwa wawekezaji wana hama kati ya hisa na hati
fungani, hii ni hulka ya kawaida ya soko na wawekezaji, pia viashiria
vingine kama market capitalization na indices karibu zote zinapanda
ukilinganisha na mwaka uliopia,” amefafanua.
Ameongeza
kuwa, “Mlinganisho wa kila wiki hasa ukizingatia kwa muktadha wa
maendeleo na uchanga wa soko letu na mauzo kwa vipindi vya muda mfupi
kama vile siku au wiki haielezi upana na uhalisia wa mwenendo wa soko.”
chanzo:Mpekuzi.
Comments