Serikali
imetangaza kutoa zawadi kiasi cha fedha kwa wananchi watakaosaidia
kutoa taarifa za siri za kuwafichua watu wanaong’oa alama za barabarani
na kuisababishia hasara kutokana na urejeshaji wake.
Ofa
hiyo imetangazwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Elias Kwandikwa, baada ya kukagua ukarabati wa eneo la Nyahua ambalo
lilikuwa limekatika kutokana na maji ya mvua na kukata mawasiliano kati
ya Itigi na Tabora.
“Meneja
wa TANROADS nafikiri tuanze kutoa kiasi fulani cha fedha kwa mtu
anayetusaidia kutoa taarifa za siri kwa watu wanaong’oa alama za
barabarani ili tukomesha tatizo” alisema Naibu Waziri kwenye hotba yake
akiwa Nyahua Uyui.
Waziri
Kwandikwa amesema lengo la kutoa fedha ni kukomesha vitendo hivyo
ambapo Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuweka alama za barabara
ili kuepuka ajali kwa watumiaji lakini baadhi ya watu wamekuwa waking’oa
alama hizo kwa ajili ya kwenda kuziuza kama vyuma chakavu.
Takribani
alama zipatazo 78 zenye thamani ya shilingi milioni 27 katika kipande
cha barabara ya urefu wa kilometa zipatazo 80.6 kutoka Tabora hadi
Nyahua wilayani Uyui zimeng’olewa.
chanzo:Mpekuzi.
Comments