Alaeddin Boroujerdi amebainisha kwamba, mipango na njama za Marekani katika Mashariki ya Kati ilikuwa ni kuzigombanisha na kuzishughulisha baina yao nchi za Kiislamu, lakini njama hizo zimegonga ukuta.
Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni ya Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyoitoa juzi huko Mash'had mbele ya hadhara ya wafanya ziara wa Imam Ali bin Mussa al-Ridha AS na kubainisha kwamba, Marekani haikuwa katika nafasi ya kukabiliana na kundi la kigaidi la Daesh bali ilikuwa katika mkondo wa kuliunga mkono kundi hilo la kigaidi.
Amesema kuwa, kushindwa Marekani huko Afghanistan ni moja ya mifano ya wazi ya kugonga mwamba siasa za Marekani katika Mashariki ya Kati.
Alaeddin Boroujerdi ameashiria uwepo wa kiushauri wa Iran katika nchi za eneo na kusema kuwa, uwepo huo daima lengo lake ni kurejesha amani na umetimia kwa ombi na matakwa ya nchi husika.
Aidha amesema kuwa, kwa kuzingatia migogoro inayoshuhudiwa hivi sasa katika Mashariki ya Kati, amani na usalama uliopo katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni neema kubwa na ni mafanikio makubwa katika faili la utendaji wa Jamhuri ya Kiislamu katika miaka 40 ya uhai wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
chanzo:parstoday.
Comments