Bashe 'Ajilipua'........Akabidhi hoja binafsi kwa Katibu wa Bunge ya kuchunguza matukio ya Mauaji na Utekaji Nchini.
Mbunge
wa Nzega (CCM), Hussein Bashe ameshindwa kuvumilia matukio mbalimbali
yanayojitokeza katika ardhi ya Tanzania na mwisho ameamua kuandika barua
yenye hoja binafsi kwa Katibu wa Bunge ili kuundwe kamati ya teule ya
uchunguzi.
"Leo
asubuhi (jana) nimewasilisha kwa Katibu wa Bunge barua ya kusudio la
kuwasilisha hoja binafsi ya kuunda Kamati teule ya Bunge kuchunguza
matukio mbalimbali yanayoonesha kutishia umoja, usalama na mshikamano wa
Taifa letu", amesema Bashe.
==> Isome barua Hiyo hapo chini
chanzo:Mpekuzi
Comments