Baadhi ya watendaji wa wizara ya afya wamekuwa wanatumia vibaya rasilimali za wizara ikiwemo dawa.

Wizara ya Afya Zanzibar imesema itahakikisha inadhibiti rasilimali za wizara hiyo ikiwemo dawa ili ziweze kuwafikia walengwa hususan kwa wagonjwa wa kifua kikuu.
Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Kifua kikuu yaliyoadhimisha Mjini Unguja ,Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Muhammed amesema kuna baadhi ya watendaji wa wizara hiyo wamekuwa wakitumia vibaya rasilimali za wizara  ikiwemo dawa jambo ambalo linachangia kuengezeka kwa maradhi Nchini.
Amesema katika kuhakikisha dawa zinawafikia walengwa Wizara hiyo itahakikisha inafatilia rasilimali zote ili zisiweza kutumika kinyume na sheria.
Akizungumzia suala la Maambukizi ya kifua kikuu Waziri Rashid amesema hali ya maradhi hayo hairidhishi kutokana na watu wengi kuuugua ugonjwa huo ambapo watu 28 elfu wanaambukizwa ugonjwa huo kila siku duniani.
Amesema suala la Udhibiti wa Maradhi ya kifua kikuu linahitaji mashirikiano  makubwa ili suala la udhibiti liweze kufikia malengo yaliokusudiwa ikiwemo kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo katika jamii.
Aidha ametowa wito kwa wananchi kuwa na utaratibu wa kupima Afya zao ili kupatiwa matibabu kwa wakati kwa lengo la kupunguza maambukizi ya maradhi jambo ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti wa maradhi hayo Nchini.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) Dk.Ghirmay Andemichael amesema ni vyema kwa Wizara hiyo kuwa na uratibu wa kuwatambuwa wagonjwa waliopo hususan wanaoishi vijijini ili waweze kupatiwa huduma za matibabu kwa wakati.
Amesema hali ya Ugonjwa huo imekuwa ikipungua kwa asilimia mbili kila mwaka jambo ambalo litaleta mafanikio makubwa pindipo litatiliwa mkazo juu ya kutolewa elimu ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.
Nae katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Asha Abdallah amesema wakati umefika kwa wananchi kufua elimu ya afya inayotolewa juu ya kujikinga na maradhi hayo ikiwemo haachana na matumizi mabaya ya Uvutaji sigara.
Amesema ni vyema kwa wananchi na viongozi wa kitaifa kuuunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana na maambukizi ya maradhi hayo ambayo yapoteza nguvu kazi ya taifa.
Siku ya kifua kikuu imedhimishwa leo Mjini Zanzibar ikiwa na ujumbe usemao TUNAHITAJI VIONGOZI MAHIRI WA KUONGOZA MAPAMBANO YA KUMALIZA KIFUA KIKUU.
chanzo:Zanzibar24.

Comments