Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki hii ya tarehe 11, Machi,
ambapo limeelezwa kwamba mwanamke huyo anayejulikana kwa jina la Jacinta
Otieno, aliwaita watoto hao ambao walikuwa wanne kwenda kunywa uji
nyumbani kwake, na ndipo alipoanza kuwacharanga na mapanga mpaka kuwaua
na kisha mwenyewe kujinyonga, huku mtoto mmoja akinusurika baada ya
kukataa kwenda kunywa uji.
Jacinta alifanya tukio hilo baada ya mke mwenzie kwenda kanisani na
kuwaacha watoto peke yao nyumbani ambako wanaishi jirani, huku mume wao
akiishi jijini Nairobi na watoto wawili ambao amewazaa yeye.
Kwa mujibu wa majirani wawili wameeleza kuwa hawakuwa na maelewano
mazuri kutokana na wivu kwa mume wao, na kwamba Jacinta alishajaribu
kutaka kujiua wiki moja iliyopita.
Watoto hao waliouawa walikuwa na umri wa miaka 7, 4 na 2, walikuwa wa mke mwenzie Hellen Otieno.
chanzo: zanzibar24.
Comments