
Kwa mujibu wa kiongozi wa eneo hilo Chief Fredrick Owino, mwanaume
huyo aliyetambulika kwa jina la Marcellus Odek, alirudi nyumbani kwake
akiwa amelewa na kuchukua jembe na kuchimba kaburi, ambalo alimzika
mtoto huyo ambaye ameelezwa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kupumua.
Taarifa zaidi zinasema kwamba mama wa mtoto huyo Annah Auma wakati
tukio linatokea alikuwa amepoteza fahamu kutokana na tatizo la kifafa
alilokuwa nalo, na alifanya tukio hilo mbele ya familia yake na
majirani, usiku wa Machi 14 mwaka huu.
Ndugu wa familia hiyo Milicent Achieng amesema mtuhumiwa aliwakuta
nyumbani na moto akiwa anapumua, kabla hajaanza kuchimba kaburi na
kumfukia, na alipoomba msaada kwa watu walikataa nakumshauri akimbie
kwani huenda angemuua na yeye.
chanzo: zanzibar24.
Comments