Zitto Kabwe: "Hili ni jambo la hatari, kama Serikali isipofanya marekebisho wabunge tusipitishe sheria hii.
Mbunge
wa jimbo la Kigoma , Zitto Kabwe amefunguka na kusema jambo ambalo
Serikali inataka kufanya kuhusu fao la matibabu litapelekea watu zaidi
ya laki sita katika mfuko wa NSSF kukosa fao hilo jambo ambalo
litaongeza shida kwa watumishi.
Zitto
Kabwe amesema hayo jana Januari 31, 2018 wakati akichangia Bungeni juu
ya mswada wa mfuko wa hifadhi ya jamii wa watumishi wa sekta ya Umma na
kuwataka wabunge kutoipitisha sheria hiyo kama Serikali haitaifanyia
marekebisho kwani kufanya hivyo ni kuwakosesha haki za kimsingi
wanachana zaidi ya laki sita wa NSSF.
"Serikali
inafanya marekebisho ya sheria ya NSSF, Sheria ya NSSF inatoa 'Health
Insurance Benifit' kwa wanachama wa NSSF lakini sheria hii ambayo
serikali inaileta hapa inaondoa 'Health Insurance Benefit' kwa wanachama
wa NSSF. Hili ni jambo la hatari, sasa hivi NSSF wanazaidi ya wanachama
laki sita kwa hiyo Serikali hii inakwenda kutunga sheria kuwaondoa watu
laki sita kwenye takwa la kisheria la Health Insurance" alisema Zitto
Kabwe
Mbali
na hilo Zitto Kabwe aliweza kutoa ushauri ambao Serikali inaweza
kuufuata ili mwisho wa siku wanachama wa NSSF waweze kupata haki yao ya
msingi ya matibabu pindi mifuko hiyo itakapounganishwa.
"Serikali
inataka 'Health Insurance' zote ziwe zinatolewa na NHIF inaeleweka
tunachopaswa kukifanya kwenye sheria ni kuweka provision inayosema
kwamba fao hilo la Health Insuarance litatolewa na NHIF kwa NSSF
kuchukua ile michango inayolipia Health Insurance na kuipeleka NHIF.
Hivyo ukiwa na kadi ya NSSF na mwanachama wa NSSF moja kwa moja unakuwa
mwanachama wa NHIF, hii ndiyo njia bora kabisa ambayo Serikali inapaswa
kufanya na nawashauru ndugu wabunge kama marekebisho haya hayatafanywa
tusiipitishe sheria hii kwa sababu tunakwenda kuwaondoa watu laki sita
kutoka kwenye 'Health Insurance'" alisisitiza Zitto Kabwe
chanzo:Mpekuzi.
Comments