Wawakilishi hao wa Ligi ya Mabingwa Afrika wataifuata St. Louis kwa mechi ya marudiano baada ya juzi Jumamosi kuishinda bao 1-0 katika mechi ya mkondo wa kwanza na sasa imepewa mchongo wa kuwaondosha Washelisheli hao.
Kinda wa Tanzania anayecheza soka huko, Hussein Kazi, ameitaka Yanga ianze kujiandaa na mazingira ya joto kali la ugenini watakaporudiana na St. Louis Februari 20.
Kazi amesema ni bora Yanga iende mapema zaidi nchini humo ili kuzoea kwa haraka hali hiyo ya hewa, kwani kwa sasa kuna joto kali kiwango cha chini ikiwa ni nyuzi joto 24 na cha juu ni 32.
“Nimekaa Dar kwani nilicheza Simba B hivyo naweza kutofautisha kiwango cha joto la Dar na kule, kama Yanga isipozingatia hili inaweza kupata wakati mgumu,” alisema.
Hata hivyo nyota huyo aliongeza kwa kusema ni bora Yanga isafiri na vyakula vyao ili kuepuka fitna za soka kwa sababu hata nchini humo zipo.
“Wanacheza kwa umakini mkubwa, sikutizama mchezo kwa sababu nipo Vietnam, nilikuwa nafanya majaribio ila nina uhakika walicheza kwa kujilinda. Hiyo ndio staili yao, mshambulizi yao huwa ni ya kustukiza,” aliongeza.
“Wanaotakiwa kuwachunga sana ni Gervais Waye-Hive anapenda kutokea pembeni na kati, pia kuna Elijah Tamboo.
Comments