Wizara ya Elimu yatoa ahadi hii kwa wanafunzi wa Zanzibar.

wizara ya elimuWizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imesema itaimarisha  miundombinu ya elimu  ikiwemo kusimamia mitaala  ili iyende sambamba na mahitaji ya wanafunzi.

Akizumgumza  Mara baada ya kufunga Mkutano wa kutathmini sekta ya elimu  uliowakutanisha wadau mbalimbali wa elimu nchni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mmanga Mjengo Mjawiri amesema  Wizara  ya elimu imekubali kuyafanyia kazi matatizo yote yanayoikumba sekta  ya elimu ambayo yametajwa kuwa ndio chanzo cha wanafunzi kutofanya vizuri katika mitihani  yao.

Mmanga amesema atahakikisha mitaala ya kufundishia inaenda sambamba na  fani za wanafunzi watazozisomea ambapo amefafanua kuwa kama mwanafunzi atakuwa anandoto za kuwa daktari au mtaalamu wa kilimo basi mitaala hiyo iweze kumuwezesha  kutimiza malengo yao.

Aidha amesema kwa masomo ya sayansi  wizara itafanya kila njia kuhakikisha kila skuli inakuwa na maabara na vifaa vya sayansi ili kuwawezesha kufanya vizuri katika masomo yao kwa njia ya vitendo ambapo lengo kuu ni kuwa na elimu bora.

Hata hivyo amesema  licha ya hayo pia watahakikisha walimu wanaajiriwa wa  kutosha  ambao watakuwa na fani zote  na wenye sifa za kufundisha ili kutimiza ndoto za vijana kuweza kufikia na kuwataka wanafunzi kuwa na bitii katika masomo yao kwani hivi sasa serikali imejipanga kuinua sekta ya elimu kwa kiwango kikubwa ili kuzalisha wasomi watakao kuwa wazalengo  na kuweza kujakuitumikia nchi yao.

chanzo: Zanzibar24.

Comments