WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku tatu kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya
wilaya ya Ukerewe Bw. Frank Bahati aeleze amepeleka wapi zaidi ya sh
milioni 350 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali.
Ametoa
agizo hilo jana (Jumapili, Februari 18, 2018) wakati akizungumza na
madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe akiwa katika
siku ya nne ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.
Waziri
Mkuu amesema Serikali haiwezi kuvumia kuona fedha inazopeleka katika
halmashauri hiyo kwa ajili ya kugharamia miradi na kulipa madai ya
watumishi zinatumika kinyume na maelekezo.
Alisema
miongoni mwa fedha hizo ni sh. milioni 451.47 za miradi ya miradi ya
maendeleo (CDG), ambapo zilizotumika ni sh. milioni 221.9 tu.” Namtaka
Mkurugenzi na Muweka hazina wa Halmashauri hii Bw. Peter Molel tarehe 21
waje Mwanza wanieleze walikopeleka fedha hizo.”
Waziri
Mkuu amesema fedha zingine ni sh. milioni 50 za ziizotolewa na Serikali
kwa ajili ya kulipa madai mbalimbali ya watumishi kama likizo ambapo
zililipwa sh. milioni 13 na zingine hazijulikani zilipo.
Pia
Serikali ilitoa sh. milioni 65 za kugharamia mradi wa umwagiliaji wa
Bugorola ambazo nazo hazijulikani zilipo pamoja na sh. milioni 84
zilizotolewa kwa ajili ya kulipa motisha kwa walimu ambapo zilizolipwa
ni sh. milioni 60 tu.
“Kama
mlidhani Ukerewe ni sehemu ya kutafunia fedha za umma mmekosea kwa
sababu Serikali haiwezi kuvumia haya, Mkurugenzi umeaminika na kupewa
dhamana ya kusimamia rasilimali za umma lakini unafanya tofauti.”
Waziri
Mkuu amesisitiza kwamba lazima viongozi hao wahakikishe fedha
zinazopelekwa na Serikali katika Halmashauri zao zikiwemo za utekelezaji
wa miradi ya afya, elimu, uvuvi zinatumika kama ilivyoelekezwa na si
vinginevyo.
Pia
Waziri Mkuu amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza asimamie
utendaji wa viongozi na watumishi katika wilaya zote za mkoa huo na
kisha kutoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa, Bw. John Mongella.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo
wasikubali kugawanywa kwa sababu ya maslahi ya watu ambayo hayana tija
kwao na hata kwa wananchi wa wilaya hiyo.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo baada ya kubaini kuwepo kwa mgogoro kati ya
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Bahari pamoja na Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo Bw. George Nyamaha ambao wamekuwa wakiwagawa watumishi.
Amewataka
viongozi hao kurekebisha tofauti zao kwa sababu mgogoro wao
umesababisha watumishi kugawanyika, hivyo kuwaumiza wananchi wa wilaya
ya Ukerewe kwa kushindwa kuwahudumia vizuri jambo ambalo halikubaliki.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, FEBRUARI 18, 2018.
chanzo:Mpekuzi.
Comments